Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano, January Makamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira wametembelea katika Dampo la Pugu, Kinyamwezi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuona jinsi ya kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira Tanzania.
Makamba amesema ujio wa Mkurugenzi huyo utasaidia ushirikiano baina ya Tanzania na shirika hilo katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuzifanya taka kuwa mali ghafi ili kuzalisha umeme kupitia taka hizo siku za mbeleni.
Amesema changamoto ya taka Tanzania imekuwa kubwa sana kutokana na kasi ya maendeleo, hivyo katika kukabiliana na tatizo hilo itatengenezwa miundombinu itakayowezesha taka hizo kuwa gesi na kupunguza uchafuzi wa mazingira.