Meneja wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amemtaka Rais wa klabu hiyo Florentino Perez, kufanikisha mpango wa usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Chelsea Eden Hazard.

Zidane amekua shabiki mkubwa wa Hazard kwa kipindi kirefu, kutokana na kukunwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye ni sehemu ya mafanikio ya Chelsea tangu alipotua Stamford Bridge mwaka 2012.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Real Madrid zimeeleza kuwa, Zidane amefuta mpango wa kusajiliwa kwa mlinda mlango wa Thibaut Courtois, na kupendekeza fungu lililotengwa kuelekezwa kwa Hazard.

Zidane anaamini bado ana nafasi ya kuendelea kumuamini mlinda mlango wake wa sasa Keylor Navas, ambaye amekua muhimili mkubwa kikosini mwake.

Juma lililopita Rais wa Real Madrid aliahidi kumuweka sokoni Navas itakapofikia mwishoni mwa msimu huu, huku akisisitiza kuwa katika mpango wa kumsaka mlinda mlango mwingine, ambaye atakua na viwango vinavyotakiwa klabuni hapo.

Mtoto wa Trump amsimamisha kazi mwandishi
Liverpool Wakubali Kumuachia Lazar Markovic