Rapper Young Killer kutoka Mwanza ameonesha kuumizwa na uchache wa vipindi vinavyozungumzia muziki wa hip hop katika vituo vya redio mbalimbali hapa nchini.

Akifanya mahojiano kupitia kipindi cha Extra Fleva cha Uplands FM, Njombe wakati akizungumzia kitu ambacho kinakosekana katika muziki wa hip hop.

Young Killer amesema muziki wa hip hop ni kama muziki wa Taarab ambao umetengewa muda maalum wa kuuzungumzia, ni vyema pia muziki wa hip hop ukatengewa muda angalau nusu saa au hata saa moja ili kuufanya muziki wa hip hop kuwa na thamani.

Akizungumzia wasanii kutaja majina ya wasanii wengine kwenye nyimbo zao kama ambayo ilitokea kwenye wimbo wake wa Sinaga Swagga, rapper huyo amesema yeye huwa hamtaji msanii kwenye wimbo wake kwa maslahi binafsi lakini anamtaja msanii kama kuna uhitaji wa kutajwa katika wimbo wake.

Majaliwa awataka NEEC kutoa mikopo yenye gharama nafuu kwa wananchi
Man Utd Wamkosa Gonçalo Manuel Ganchinho Guedes