Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha Dawati la Ulinzi la na Usalama katika shule zote  pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi ya Kata na Vijiji Nchini kote ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Sihaba Nkinga, amesema hayo wakati akiongea katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu cha Baraza la Watoto la Taifa kinachofanyika kwa siku mbili Mjini Morogoro.

 

Aidha amewataka wajumbe wa Kikao hicho kujadiliana kwa kina juu ya ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na kuwasilisha mapendekezo yao Wizarani  akisema kuwa hivi karibuni vitendo hivyo vimeongezeka kwa wingi sana katika Jamii.

 

Amesema kuwa kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa Mpango Mkakati wa Kupambana na Kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa miaka mitano Serikali itahakikisha vitendo vya ukatili vinapunguzwa kwa asilimia hamsini kupitia mpango kazi huo na kuongeza kuwa vitendo vya ukatili kwasasa vinatofautiana viwango akitaja ukatili huo kuwa ni ubakaji, ulawiti, ukeketeji, mimba na ndoa za utoto

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa  Caroline Augustino,amewataka wasichana walio katika umri mdogo kuachana na tamaa zinazowapelekea kujiingiza katika matendo mabaya yanayosababisha kukatisha ndoto zao ikiwemo kushindwa kuendelea na masomo pamoja na kujikuta wanapata ndoa za utotoni na kuwataka wazazi na walezi kutambua kuwa mtoto wa kike ana fursa sawa na watoto wakiume hasa kwa jamii za vijiini.

Hata hivyo Caroline amezitaka jamii za wafugaji na badhi zilizoko kanda ya ziwa kuacha tabia ya tohara mbili kwa watoto wa kiume na tohara kwa watoto wa kike akisema tohara kwa wanawake inasababisha vifo na maumivu ambayo huleta hathari mbaya kwa wanawake kwa kipindi kirefu.

Kakao cha Baraza Kuu la Watoto Taifa pamoja na mambo mengine kinakutana kujadili kuandaa Mkutano Mkuu wa Baraza la Watoto Taifa utakaofanyika Mwezi Aprili Mwaka huu

Nay wa Mitego: Ukitaka shindana na mimi jiandae kufirisika, karibu mjengoni Free Nation Records
Chakua watoa neno kwa serikali kuhusu matumizi ya elektroniki sekta ya usafirishaji