Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limemtaka kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, ajisalimishe kwa kupeleka vibali ili kuondoa utata  wa gari alilokuwa akilitumia katika kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22, mwaka huu wilayani kahama.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Shinyanga Elias Mwita, amesema kuwa kiongozi huyo anasakwa kutokana na kuwapo kwa taarifa za intelijensia zianazoelezea kuwa anatumia gari ambalo halikuwa na vibali.

Mwita amesema kuwa Jeshi hilo linamtaka Zitto apeleke taarifa kuhusu gari analomiliki aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo hakulitaja namba za usajili.

“Siku ya kufunga mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Isagehe Wilayani Kahama, tulipata taarifa kwamba Kabwe anatumia gari ambalo si halali, halina vibali, tukafikiri tumpate baada ya matukio atupe maelezo kuhusu gari analomiliki,”amesema Mwita.

Hata hivyo amesema kuwa Jeshi la polisi linamtaka kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo apeleke vibali vya gari hilo na ndiyo kitu ambacho wanakihitaji.

Robert Pires Amuhoji Sanchez, Abaini Ukweli Wa Mambo
Joleon Lescott Arudi Kwa David Moyes