Kufuatia hitilafu zilizojitokeza katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme uliopo eneo la Ubungo jijini Dar es salaam, tayari wataalam wa Tanesco wameshagundua na marekebisho yameanza huku baadhi ya maeneo yameshapatiwa umeme, pia maeneo mengine zaidi yakitarajiwa kufikiwa na huduma hiyo mapema baada ya marekebisho kukamirika.
Taarifa hizo zimetolewa na Grory Kiondo wa Tanesco wakati akifanya mazungumzo na Dar24 hivi punde ambapo amesema kuwa hitilafu hiyo imesababisha kukatika kwa umeme katika maeneo ya Dar es salaam na Pwani na wala si Tanzania nzima.
Umeme ulikatika leo saa 12:32 asubuhi katika mtambo wa kilovolti 220 ambao ni wa kupoozea na kusambaza umeme uliopo Ubungo lakini kwa kuwa wataalam wameshagundua,” Muhaji ameambia Mwananchi.
Naye Kaimu meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema wataalam wanaendelea kushughulikia tatizo hilo.