Benki ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Makhtar Diop.

Amesema kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Bandari hiyo kutasaidia kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na Bandari hiyo hatua itakayo chochea ukuaji wa  uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika  Makhtar Diop, amesema kuwa Benki yake imefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kukuza uchumi na kwamba Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yana fikiwa kwa haraka

Aidha, Makhtar ameishauri Serikali kuongeza ushirikiano kati yake na Sekta Binafsi katika kuchochea  biashara na uwekezaji pamoja na kutupia jicho sekta ya kilimo kwa kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuondokana na umasikini na kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo

Jafo awashangaa wanasheria wa Halmashauri kushindwa kesi
Mchezaji Kenya apata usajili China