Wawakilishi wa Afrika mashariki kwenye fainali za Afrika (AFCON 2017) zinazoendelea nchini Gabon, timu ya taifa ya Uganda wamemaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kuambulia matokeo ya sare dhidi ya Mali.

Uganda ambao tayari walikua wameshatupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa na Misri pamoja na Ghana katika kundi hilo, walionyesha ukakamavu mbele ya Mali na kuambulia point moja ambayo itaendelea kubaki kwenye kumbukumbu zao.

Bao la Uganda katika mchezo huo lilifungwa na Farouk Miya katika dakika 70, lakini dakika tatu baadae Mali walisawazisha kupitia kwa Yves Bissouma.

Sare hiyo imeendelea kuifanya Uganda kuwa wa mwisho kwenye msimamo wa kundi D kwa kupata Point moja, wakitanguliwa na Mali wenye point mbili na Ghana wamemaliza wakiwa katika nafasi ya pili huku Misri wakiongoza kwa kumiliki point 7.

Uganda imeshiriki kwa mara ya sita katika fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kufanya hivyo katika miaka ya 1962, 1968, 1974, 1976, 1978 na 2017.

Copa del Rey: Real Madrid Yatupwa Nje
AFCON 2017: Mohamed Salah Aipeleka Misri Robo Fainali