Vinara wa ligi kuu ya soka nchini Hispania Real Madrid, wametolewa kwenye michuano ya kombe la Mfalme (Copa del Rey) baada ya kuambulia matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Celta Vigo.

Real Madrid walikwenda katika uwanja wa ugenini usiku wa kuamkia hii leo, huku wakiwa na kovu la kufungwa mabao mawili kwa moja kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao uliunguruma juma lililopita.

Mabao ya Celta Vigo katika mpambano wa mkondo wa pili yalifungwa na Danilo Luiz da Silva aliyejifunga katika dakika ya 44 na Daniel Wass dakika ya 85, na kwa upande Real Madrid  Cristiano Ronaldo na Lucas Vazquez walifunga katika dakika ya 63 na90.

Kwa matokeo hayo, Celta Vigo wametinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mfalme (Copa del Rey) na sasa wanasubiri ratiba ya hatua hiyo.

Wakati huo huo Atletico Madrid nao wametinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kulazimisha matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Eibar.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Atletico Madrid walipata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri, hivyo wamesonga mbele kwa jumla ya mabao matano kwa mawili.

Hii leo michuano hiyo inaendelea tena kwa michezo mmoja ambapo.

FC Barcelona Vs Real Sociedad

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza FC Barcelona walipata ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Watu wanne wauawa kwa kupigwa risasi
AFCON 2017: Uganda Waambulia Sare