Bingwa wa mbio za mita 100 upande wa wanaume Usain Bolt atalazimika kurudisha dhahabu moja miongoni mwa dhahabu tisa alizoshinda baada ya mwanariadha mwenza Nesta Carter kupatikana alitumia dawa za kusisimua misuli.

Carter alikuwa miongoni mwa wanariadha wanne wa Jamaica walioshinda mbio za mita 100 kupokezana vijiti katika michezo ya beijing 2008.

Pia ni miongoni mwa wanariadha 454 waliochukuliwa vipimo vyao na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC mwaka uliopita na amepatikana alitumia dawa ya aina ya methylhexaneamine.

Bolt alishinda dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400 kupokezana vijiti na kuongeza mafanikio yake katika mbio hizo mwaka 2008 na 2012.

EFL CUP: Southampton Yaibanjua Liverpool
Watu wanne wauawa kwa kupigwa risasi