Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Itikadi na Uenezi), Hamphrey Polepole amefichua siri akisema kuna watu wanakihujumu chama hicho kwa makusudi.

Amesema mfano mzuri ambao unadhihirisha kuwa chama hicho kinahujumiwa ni pale sukari ilipoadimika, ambapo baadhi ya wafanyabiashara walificha bizaa hiyo kwa lengo la kuuza kwa gharama kubwa.

“Tunahujumiwa,Rais alipoanza kazi lilikuja jambo la sukari hii ilikiuwa hujuma kabisa lakini hakuna mtu anasema, sasa nawaomba niynyi (New Habari) muwe wa kwanza kusema,ifike mahari tuweze kujitenga na rafiki mwizi,”amesema Polepole.

Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kutembelea Kampuni ya New Habari (2006) Limited, amesema rais alipokuja alisema Tanzania ya Viwanda na msingi wake ulikuwa ni kulinda viwanda vya ndani ambavyo vinaajiri watu kwa sababu ya teknolojia yetu iko chini.

Katika hatua nyingine, Polepole amemuonya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wa (ACT-Wazalendo) kutokana na kauli yake ya kwamba ataweka ubunge wake rehani kama Serikali itamuonesha tani milioni 1.5 za mahindi.

Goncalo Guedes Atua Rasmi Parc des Princes
AY amuweka Joh Makini juu ya rap ya Bongo kwa walioishi humo miaka 9