Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu, Zelote Stephen amewaagiza wakurugenzi, waratibu wa Tasaf, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji Mkoani humo kuhakikisha kwamba haki inapatikana katika kufanya mchujo kwa zile kaya ambazo hazistahili kuingizwa katika mpango wa kuzinusuru kaya masikini (TASAF)

Zelote ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara yake ya siku ya nne katika wilaya za kalambo na Nkasi Mkoani humo kwa kuzitembelea kaya za walionufaika na mpango wa TASAF ambao bado wanaendelea kunufaika na wale ambao waliondolewa katika mpango huo baada ya kukosa vigezo na hatimae kutakiwa kurudisha pesa hizo.

“nimezunguka nimebaini kuwa zoezi hili limekuwa likifanyika hovyo hovyo, hakuna umakini, hakuna usimamizi, hakuna ufuatiliaji, matokeo yake kwenye mradi wameingizwa watu wenye sifa na wasio na sifa, Wakurugenzi na waratibu wasimamie zoezi hili, wasiwaachie wenyeviti na watendaji wa vijiji peke yao katika hili,”

“Wale wote ambao hawana vigezo na kweli ionekane kwamba hawana vigezo vya kuwepo basi watolewe kwasababau sehemu zingine utakuta kwenye mpango huo wameingizwa wastaafu, mke wa mwalimu, mjumbe wa smc yumo humo humo, hii haifai,” Zelote alifafanua.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa wa Rukwa, James Kapenulo amesema kuwa kaya zote ambazo zilinufaika na TASAF kwa kuwa na mashamba na nyumba nzuri ambazo kabla ya TASAF hawakuwa nazo, familia hizo ndio ziwe za mfano na ziendelee kuwezeshwa ili tathmini itakapokuja kufanywa ioneshe hali halisi ya mafanikio ya mpango huo.

“Hatuwezi tukaendelea kuwaweka wale ambao wakipewa pesa za TASAF wanaishia kwenye vilabu vya pombe na kumuacha yule ambae akipewa pesa hizi ananunua kuku au mbuzi au bati na kuwapeleka watoto shuleni, hayo sio madhumuni ya mpango huu, huyu aliyefanikiwa baada ya TASAF ndiye ametoka weye umaskini.

 

Vanessa aitaja Simu chanzo cha kugombana na Jux
Alshabaab wadai kushambulia kambi ya jeshi la Kenya