Waziri Mkuu, Kassim majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini kuacha tabia ya kudokoa fedha za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri zao kwa sababu Serikali iko macho na itawashughulikia wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

“yeyote aliyeletwa Ludewa akidhani amekuja Wilaya ya pembezoni na kwamba tunaleta fedha unafanya mambo ya hovyo, nitakufa na wewe…,” amesisitiza

Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Aidha, Majaliwa ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na upotevu wa sh. milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri Ludewa.

 

Video: Ole Sendeka aagizwa kuichunguza NJUWASA
Aitor Karanka: Tutamsajili Jese Rodriguez