Marekani imetaja orodha ya mataifa sita ambayo raia wake hawaruhusiwi kupewa visa za Marekani kuwa ni Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen, mikakati hiyo mipya ikilenga kuzuia Waislamu walio na itikadi kali kutoingia kabisa Marekani.

Agizo hilo limetolewa na Rais mpya wa Marekani Donald Trump ambapo pia amepiga marufuku wakimbizi wote kutoka Syria kuingia Marekani hadi utakapowekwa mkakati mkali zaidi wa kuwakagua wakimbizi wanaotafuta hifadhi nchini humo.

Trump amesema kuwa wakimbizi wote wanaofika mipakani mwa Marekani kwa sababu ya kutoroka vita makwao au sababu yoyote nyengine pia hawataruhisiwa kwa sasa kwani maafisa wa uhamiaji wamepewa miezi minne ya kuweka mfumo huo wa upekuzi na ukaguzi wa kina anaouita “extreme vetting”

 

Rais Magufuli ahudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika(AU)
Jenerali Colley wa Gambia akamatwa akitoroka