Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameondoka nchini na kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ambako atahudhuria Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Magufuli kutoka nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano.
Aidha,taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam imesema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameagwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Wengine waliojumuika kumuaga Rais Magufuli ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda.
Hata hivyo, pamoja na kuhudhuria mkutano huo, akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria mkutano huo.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 29, 2017
Trump azuia mataifa sita kuingia Marekani