Wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi Geita kwa zaidi ya siku tatu wameokolewa wakiwa hai na utaratibu wa huduma ya kwanza unaendelea. Wachimbaji hao walifukiwa na kifusi walipokuwa katika shughuli zao za kila siku mgodini hapo. Wachimbaji hao wamekaa zaidi ya saa 100 chini ya ardhi na kuzua taharuki kwa ndugu na jamaa zao ambao walikuwa wamekusanyika eneo la mgodi huo wakihofia ndugu zao kupoteza maisha. Tazama hapa picha za tukio la uokoaji

Wachimbaji 15 waokolewa wakiwa hai mkoani Geita
Mwita ahimiza upendo kwenye huduma za afya