Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa bado anaamini atakuwa Rais wa Zanzibar akidai kwamba nchi alizopeleka malalamiko yake zimefikia katika hatua nzuri.
Tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2015, Maalim Seif amekuwa akitoa kauli za mbalimbali za matumaini akisema Mambo yanaelekea kuwa mazuri.
Hata hivyo, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein aliyeshinda katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016 ambao Maalim Seif aligoma kushiriki, amesema kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kumwondoa madarakani, awe wa ndani au nje ya nchi.
Ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha televisheni, Maalim Seif amesema wananchi wasifikiri kuwa mataifa hayo yamenyamaza, bali suala hilo litapatiwa ufumbuzi na atapata haki yake hivi karibuni.