Jose Mourinho ameindoa Man Utd katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini England (PL) kwa msimu huu 2016/17.
Mourinho alitangaza kukiondoa kikosi chake katika mchakato huo, mara baada ya ushindi wa mabao manne kwa sifuri walioupata jana kwenye mchezo wa mzunguuko wa tano wa kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic.
Mourinho alisema ni uwendawazimu kuendelea kuufikiria ubingwa wa England katika kipindi hiki, kutokana na kasi ya kikosi chake kuwa ndogo, tofauti na ilivyo kwa klabu ambazo zimemtangulia kwenye msimamo wa ligi kuu.
Alisema kutwaa ubingwa ni mipango ambayo inatakiwa kusukwa kisawa sawa na kwake anaamini suala hilo kwa Man utd halipo kwa msimu huu.
Kuhusu michuano mingine ambayo Man Utd wanaendelea kushiriki kama kombe la ligi (ELF Cup) na kombe la FA, Mourinho alisema kwa upande huo amejiwekea malengo makubwa ya kupambana na ikiwezekana kutwaa ubingwa.