Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo amezindua programu maalumu ya kushiriki kwenye mashindano ya ya olympic.
Programu hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Karume jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ambapo itasaidia kuwajengea uwezo wachezaji.
Aidha rais wa shirikisho hilo amesema programu hiyo itahakikisha Tanzania inashiriki fainali za olympic na kombe la dunia mwaka 2026,na kuwashukuru wadau wote wanashirikiana na Shirikisho hilo.
Amesema hazina ya vijana waliopo ni ushahidi tosha kwamba programu hii itakuwa ni chachu kubwa ya kupata timu imara ya taifa chini ya miaka 23 na ameiomba Serikali kuisaidi TFF.