Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi Ofisi za wizara yake mkoani Dodoma na kuwataka Watumishi wa wizara waliohamia Makao Makuu ya Serikali, Dodoma kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa.

Mwakyembe amezindua rasmi makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria yaliyopo mkoani Dodoma katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya wizara hiyo na watumishi wake 31 kuhamia rasmi makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.

Aidha, Mwakyembe amesema kitendo cha kuhamia mkoani Dodoma ni utekelezaji wa agizo la kuhamia makao makuu ya Serikali ambalo lilitolewa mwezi Julai mwaka 2016 na hivyo watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi kama walivyokuwa Dar es salaam.

Hata hivyo, uzinduzi huo umehudhuriwa na Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mkuu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kanda ya Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma, Prof Kikula na watumishi 31 wa wizara ambao wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo la Serikali.

 

Serikali yatenga bil.13.9 kwaajili ya kujenga nyumba za waalimu
David Moyes Awasajili Wengine Kutoka Everton