Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inafanya operesheni ya kuondoa mabango yaliyobandikwa sehemu mbalimbali za Manispaa hiyo na kupiga marufuku ubandikwaji holela uliokuwa umekithiri na kuwataka wanaofanya hivyo wafuate taratibu zilizowekwa.

Hayo yasemwa na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu wakati akizungumza na waandishi leo Januari 31, 2017 Jijini Dar es salaam, amesema kuwa mapato ya mabango yanapotea kutokana na watu ambao hawataki kufuata utaratibu uliowekwa wa kujiandikisha na kupewa vibali.

“Mapato ya mabango ya mwaka 2016/17 tunatarajia kukusanya bilioni 10, ndio maana tunawataka hawa wahusika wa haya mabango wafuate utaratibu ili tuweze kukusanya kodi na kufikia malengo yetu tuliyojipangia katika Manispaa ya Ilala,”amesema Tabu.

Aidha, ameongeza kuwa malengo hayo ndiyo ambayoa yanawezesha kutimiza kile ambacho wamejipangia,pia amewakumbusha wale wote wanaodaiwa kulipa madeni yao kwa muda na si kulimbikiza kitu ambacho huwa kinaljeta usumbufu wakati wa kudaiwa.

Serikali: Uzalishaji wa chakula utafikia tani milioni 3
Serikali yajipanga kuhakikisha hali ya chakula ni nzuri nchini