Mshambuliaji Asamoah Gyan ana matarajio mkubwa ya kucheza mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Afrika dhidi ya Cameroon utakaounguruma hii leo mjini Franceville nchini Gabon.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Shanghai SIPG anaecheza Al Ahli Club ya falme za kiarabu kwa mkopo, alifanyiwa vipimo vya afya na alionekana yupo fit kucheza mchezo wa nusu fainali.

Asamoah mwenye umri wa miaka 31, aliumia kiazi cha mguu wakati amchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Misri, na alizua hofu ya kutokucheza tena katika fainali za AFCON za mwaka huu.

“Madaktari wetu bado wanaendelea kumpatia huduma za kitabibu, tunaamini mambo yatakua sawa saa chache kabla ya mchezo wetu dhidi ya Cameroon,” Alisema kocha msadizi Maxwell Konadu wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

“Hatuwezi kuthibitisha kwa asilimia 100 kuhusu kucheza kwake ama kutokucheza, tunasubiri kupata taarifa sahihi kutoka kwa madaktari, na kama atacheza mtamuona kwenye kikosi kitakachokua tayari kupambana na Cameroon.”

Asamoah ambaye ni mchezaji mashuhuri nchini kwao Ghana, tayari ameshafunga bao moja katika fainali za AFCON za mwaka huu.

Alifunga bao hilo wakati wa mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Mali, ambao walikubali kutandikwa bakora moja kwa sifuri.

AFCON 2017: Mwamuzi Bora 2016 Kuamua Ghana Vs Cameroon
Aliyekuwa mfungwa ateuliwa kuwa waziri wa fedha Gambia