Amadou Sanneh, aliyefungwa kwa tuhuma za kuonekana ni mpinzani wa kisiasa wa kiongozi wa zamani Yahya Jammeh, ameteuliwa kuwa waziri wa fedha katika baraza jipya la mawaziri, chini ya utawala wa raisi wa sasa Adama Barrow mara baada ya kuachiliwa huru.

Kati ya wafungwa walioachiliwa huru hivi karibuni nchini Gambia, ni miongoni mwa watakaounda baraza jipya la mawaziri ambapo tayari mawaziri wengine tisa wamekwisha kula kiapo chao, akiwemo waziri mpya wa mambo ya nje wa Gambia , Ousainou Darboe, ambaye naye alikuwa mpinzani mkubwa wa utawala wa bwana Jammeh , ambaye pia alishawahi kufungwa na utawala uliopita.

Mawaziri wengine nane ambao bado hawajajaza nafasi katika baraza la mawaziri bado hawajafahamika.

Jammeh alikuwa Rais wa Gambia tangu 1994, aliondoka nchini Gambia na kuelekea uhamishoni mwezi uliopita kufuatia kushindwa kwa uchaguzi uliofanyika mwezi December mwaka wa jana na Adama Barrow kuibuka mshindi.

AFCON 2017: Asamoah Gyan Aibua Matumaini
AFCON 2017: FECAFOOT Waongeza Morari Ya Wachezaji