Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, leo amezindua Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya  Mazingira Nchini

Makamba amesema Uzinduzi wa Mfuko na Bodi hiyo utasaidia upatikanaji wa fedha za usimamizi wa Mazingira Nchini.

“Ni matarajio yangu tutafanya kazi pamoja kuhakikisha mfuko unakuwa na fedha ya kutosha na unafanya kazi ili kukidhi malengo yaliyodhamiriwa hususan uboreshaji wa mazingira nchini” Amesema Waziri Makamba.

Amesema  uteuzi wao una maana kubwa na kuwataka wajumbe wa Bodi hiyo kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha kuwa Hifadhi ya Mazingira inakuwa ni ajenda ya kitaifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Ali Mufuruki amemhakikishia Waziri Makamba kuwa yeye na wajumbe wa bodi yake wako tayari kufanya kazi hiyo kwa heshima kubwa na kuhakikisha kuwa hifadhi na usimamizi wa mazingira unakua endelevu.

Bodi hiyo inaongozwa Ali Mufuruki, ambaye Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kampuni ya Infotech, Mwajuma Mbogoyo, Imelda Teikwa, Profesa Razak Bakari Lokina na Hatibu Senkoro. Wengine ni Alesia Mbuya, Baraka Juma Kalangahe, Dkt. Andrew Komba na Profesa Yunus Mgaya.

 

 

Paco Gonzalez: Usajili Wa Dybala Ni Hatari Kwa Rodriguez, Benzema
Majaliwa: Rais hajatangaza kufuta vyama vya upinzani