Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kwa kuwasimamisha kazi askari Polisi wenye tuhuma za bishara ya madawa ya kulevya.
Rais magufuli amesema hayo leo Februari 6, 2017 Ikulu katika hutuba fupi mara baada ya kuapishwa kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Samweli Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini DRC, Paul Meela pamoja na wengine
Amesema vita ya madawa ya kulevya si ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda peke yake bali ni vya watanzania wote.
Hivyo amepongeza harakati za mapambano dhidi ya madawa ya kulevya huku akitaka mapambano hayo yaendelee bila kujali umaarufu wa mtu yeyote yule. “hata hao wadogo wakishikwa wabanwe mpaka waeleze ni nani anawauzia” – Rais Magufuli
Rais Magufuli ameagiza pia kesi za madawa ya kulevya zisichelewe kusikilizwa mahakamani.