Wabishi wa mjini Milan nchini Italia, klabu ya Inter Milan wamepanga kuingia katika vita ya kumuwania mshambuliaji wa kutoka nchini Argentina na Man City Sergio kun Aguero ambaye anakabiliwa na tetesi za kuingizwa sokoni itakapofika mwishoni mwa msimu huu.
Aliyekua kiungo na nahodha wa Inter Milan Javier Zanetti anatajwa kuongoza mpango wa usajili wa Aguero, kutokana na kuamini ukaribu uliopo baina ya watu hao unaweza kuiletea faida The Narazzuri.
Aguero anatajwa kuwa katika wakati mgumu wa kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Man City, kufuatia ujio wa mshambhliaji kinda kutoka nchini Brazil Gabriel Jesus, ambaye tayari ameshaanzishwa kwenye kikosi cha kwanza mara mbili.
Inter Milan wanaamini ushindani wa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 utakua na changamoto kubwa, lakini bado wanajiaminisha maelewano yaliopo kati ya Zanetti na Aguero yatafanikisha amza wanayoikusudia.
Klabu za Real Madrid, FC Barcelona pamoja na Paris Saint-Germain nazo zinatajwa kuwa kwenye harakati za kuingia vitani kuiwania saini ya mshambuliaji huyo.