Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amekabidhi hati miliki za ardhi 1,361 kwa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Lukuvi amegawa hati hizo na kuwasisitiza wananchi wa wilaya ya Mvomero kuhakikisha wanapata hati za umiliki wa ardhi pamoja na kuwataka viongozi wa vijiji kote nchini kuhakikisha wanakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji kuendelea katika maeneo yao.
AIdha,Lukuvi pia amemtaka Mkuu wa mkoa wa Morogoro aainishe mashamba mengine makubwa yasiyoendelezwa na kugeuka kuwa mashamba pori ili amshauri Rais kuyafutia umiliki wa mashamba hayo na kurudishwa kwao ili kuweza kuwapa kaya maskini ambazo zinaishi katika maeneo ya hayo.
Hata hivyo,amesema kuwa wakati wa kampeni mwaka 2015,Rais Dkt. John Magufuli aliahidi wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika maeneo yote ya nchi kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa, na kwa miaka mitano takribani vijiji 7,500 vitapimwa kwa kupangwa kila halmashauri 25 ambapo na kila mwaka vitapimwa vijiji 1,500 na kutoa hati. pia amesema kuwa zoezi la upimaji linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika kuondoa migogoro inayojitokeza