Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe amekanusha tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuhusu kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Mbowe amesema kuwa yeye hajawahi kujihusisha wala kutumia madawa hayo ya kulevya na amekituhumu Chama Cha Mapinduzi kuwa ndio wahusika wakubwa wa biashara hiyo.

Amesema kuwa Chama cha Mapinduzi na washirika wake ndio wahusika wakubwa wa biashara hiyo ya madawa ya kulevya ndio maana walikuwa kimya kwa mda mrefu, huku wakiona taifa likiangamia.

Aidha, amesema kuwa vita ya kuzuia madawa ya kulevya ambayo watanzania wengi wamefungwa nchi mbali mbali duniani lakini serikali imekaa kimya.

Video: Taarifa ya Polisi kuhusu Askofu Gwajima na Manji
Rada Za Inter Milan Zaelekezwa Kwa Alexis Sanchez