Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa bunge bado halijapoteza hazi liliyonayo na bado heshima yake iko palepale.

Amesema kuwa Bunge halina ugomvi wowote na Serikali wala Mahakama, kwakuwa kila kitu kina nafasi yake, na kuongeza kuwa maofisa kujisahau na kuvuka mipaka ya kazi zao ni lazima wajirekebishe.

Ndugai amesema kuwa kama viongozi wataendelea kufanya kazi kibabe bila kufuata utaratibu basi nchi itavurugika na jambo lolote likitaka kufanyika linalowahusu Wabunge basi ni lazima wafuate utaratibu wa kutoa taarifa kwa Spika.

Ndugai amefikia hatua hiyo mara baada kamata kamata ya wabunge ambayo imeanza kujitokeza hivi karibuni bila kufuata utaratibu wa kutoa taarifa kwake, kwa kuwa yeye ndiye kiongozi wa bunge hilo.

Goodluck Mlinga: Vita ya madawa ya kulevya imeanza kwa ugomvi binafsi
Video: Waziri Mwigulu atoa neno kuhusu sakata la madawa ya kulevya