Gwiji wa soka nchini Nigeria Samson Siasia ameonyesha dhamira ya kurejea kwenye ukufunzi wa mchezo huo barani Afrika, kufuatia mataifa kadhaa kusaka makocha watakao kabidhiwa jukumu la kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 na zile za AFCON za mwaka 2019.

Siasia ambaye amekua nje ya ukufunzi wa soka tangu alipoachana na kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria chini ya umri wa miaka 23 kilichotwaa medali ya shaba ya fedha wakati wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2016, juma lililopita alitajwa kuwa sehemu ya makocha 52 walioomba kazi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda.

Jina la kocha huyo pia limejitokeza katika orodha ya watu wanaowania nafasi ya kukinoa kikosi timu ya taifa ya Afrika kusini ambacho kwa sasa hakina kocha mkuu, baada ya kutimuliwa kwa Ephraim Mashaba tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Mpaka sasa makocha 32 wameshawasilisha maombi ya kuwania ukuu wa kiti cha benchi la ufundi la Afrika kusini.

Jina lingine ambalo limeonekana kwenye orodha hiyo ni la aliekua meneja wa klabu ya Man City, Inter Milan na  Galatasaray  Roberto Mancini, aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Giovanni Trapattoni pamoja na Hassan Shehata ambaye alikisaidia kikosi cha Misri kutwaa ubingwa wa AFCON mwaka  2006, 2008 na 2010.

Bongo muvi kuoneshwa cinemax Mlimani city
TID aomba radhi kwa kutumia ‘Unga’, awapa neno wanaohofia atawataja