Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amempongeza Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimama imara katika kupiga vita madawa ya kulevya.
Ameyasema hayo mapema hii alipokuwa akizungumza na watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam, amesema kuwa vita ya kupigana na madawa ya kulevya ni vita kubwa na wala sio ya kawaida kwa kuwa inakufanya uwe na hofu ya usalama.
Amesema kuwa vita ya madawa ya kulevya imekuwa ndogo na nyepesi mara baada ya Rais Magufuli kuunga mkono na kusimamia kikamilifu kitu ambacho kinaifanya iwe nyepesi.
Aidha, Makonda ameongeza kuwa madhara yanayoikumba jamii yanayosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya ni makubwa zaidi kuliko jinsi watu wanavyofikiria.
Hata hivyo, Makonda amewashangaa wale wanaopinga mapambano dhidi ya madawa ya kulevya bila kuangalia madhara yatokanayo na madawa hayo.