Kocha wa mabingwa wa soka Afrika kusini Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane amekiongezea nguvu kikosi chake kwa kumsajili beki wa kushoto kutoka nchini Algeria Fares Hachi akitokea ES Setif.

Mamelodi Sundowns wamemsajili mchezaji huyo kwa kumsainisha mkataba wa miaka minne, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja baadae, endapo ataonyesha juhudi zitakazolivutia benchi la ufundi la mabingwa hao wa barani Afrika.

Kabla ya kufanikisha mpango wa kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo, Hachi mwenye umri wa miaka 26, alipata nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha Mosimane, kwa idhini ya klabu yake ya ES Setif.

Hachi anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Sundowns ambacho kitacheza mchezo wa Absa Premiership dhidi ya Bloemfontein Celtic utakaochezwa Dr Petrus Molemela Stadium mjini Bloemfontein kesho usiku.

Hachi‚ alicheza dhidi ya Sundowns wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika mwaka 2016, akiwa na klabu yake ya zamani ya ES Setif, na hapo ndipo Mosimane alipoanza kuvutiwa na kiwango chake.

Wakati huo huo Sundowns wamethibitisha kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo Anthony Laffor ambaye anakua mchezaji wa pili kufanya hivyo, baada ya mlinda mlango Denis Onyango kusaini mkataba wa miaka minne juma lililopita.

Marco Verratti, Gerard Pique Kurejea Dimbani Leo
Sadio Mane Amwachia Majanga Mjomba Wake