Awamu  ya mazungumzo ya kutafuta Amani nchini Burundi yanatarajiwa kuanza Alhamisi mjini Arusha, Tanzania chini ya usimamizi wa rais mstaafu wa Tanzania Benjamini William Mkapa.

 Serikali ya Burundi bado haijatangaza majina ya wajumbe wake katika mazungumzo hayo na hivyo kuzusha wasiwasi kuhusu kuhudhuria kwao.

Aidha, Mazungumzo hayo yamelenga kufikia mkataba wa kumaliza mzozo wa kisiasa unaoikabili Burundi tangu rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kugombea awamu ya tatu katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Allain Aime Nyamitwe, amesema kuwa ni mapema mno kujuwa wajumbe wa serikali katika mazungumzo hayo.

Hata hivyo kauli hiyo imezua wasiwasi iwapo Serikali ya Burundi itashiriki au la katika kikao hicho ambacho Serikali wanasema hawawezi kukaa kwenye meza moja na wanasiasa wa upinzani ambao tayari wamealikwa na Ofisi ya mpatanishi.

Wajumbe zaidi ya 30 kutoka maeneo yote wamealikwa lakini hatua ya msimamizi wa mazungumzo hayo ya kualika wanasiasa wanaofuatiliwa na vyombo vya sheria Burundi imeanza kulaaniwa na mashirika ya kiraia yaliokaribu na chama tawala.

Kesi ya uchochezi inayomkabili Tundu Lissu yafikia patamu
Mwakyembe: Kwa Serikali hii tutashinda vita ya madawa ya kulevya