Mshambuliaji mpya wa klabu ya Man City Gabriel Jesus yupo kwenye hatari ya kukosa michezo iliyobaki kwa msimu huu, kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya AFC Bournemouth, uliochezwa usiku wa kuamkia jana.
Majibu wa vipimo alivyofanyiwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Brazil, yameonyesha huenda akakaa nje ya uwanjani kwa miazi miwili hadi mitatu.
Mchezo dhidi ya AFC Bournemouth ulikuwa mchezo wa tatu kwa Gabriel tangu alipokamilisha taratibu za uhamisho wake akitokea nchini kwao Brazil mwezi Januari mwaka huu.
Majibu ya vipimo, yamemsikitisha meneja wa Man City Pep Guardiola ambapo amesema ni vigumu kuamini, lakini hana budi kukubalina na hali halisi.
Amesema itamlazimu kusubiri na kuona kama atakuwa na uwezo wa kumtumia tena Gabriel kabla ya msimu huu kufikia kikomo mwezi Mei, kwani alimini ujio wake ulikua umeleta chachu mpya ya ushindani kikosini mwake.
Hata hivyo amemtakia kila la kheri mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, katika kipindi hiki ambacho atakitumia kwa kujiuguza jeraha la kifundo cha mguu.
Gabriel ambaye alisajiliwa na Man city kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 27 akitokea Palmeiras, tayari alikua ameshaifungia The Sky Blues mabao matatu katika michezo mitano aliyocheza.