Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, atoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya  na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.

Akiongea Jumatano hii katika kipindi East Africa Breakfast cha EA Radio, Ridhiwani ameishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa.

Ameeleza kinagaubaga, vita dhidi ya madawa ya kulevya ni agenda ya Taifa nzima, ijapokuwa mwisho wake ni mgumu kwani hata ukiangalia nchi zilizo endelea kiuchumi kama Marekani bado zinapambana na vita hii takribani miaka 80 sasa.

“Kwanza nataka kusema hii vita ni jambo jema sana, unajua jamii yetu hasa hasa kama hayajakukuta kwenye familia yako huwezi kuelewa ukubwa wa tatizo na madhara yake, Kwa mfano mimi katika maeneo ambayo naishi, kuna watu ambao walikuwa katika umri wetu tumewapoteza, kwa mmfano vijana kama akina Langa wale, tumejaribu kuwasaidia mpaka ikaonekana hakuna njia ambayo unaweza ukawasaidia tena, sisi kwetu tunaumia kwa kuona hawa vijana walikuwa na future nzuri sana”. amesema Ridhiwani Kikwete.

Amewaomba watanzania kutoa ushirikiano wa dhati kwa timu iliyoundwa ya kutokomeza madawa ya kulevya kwani anaamini kupitia ushiriakiano huo Sianga na timu yake itafanya vizuri katika vita hii.

”Bwana Sianga ambaye kwangu mimi ni mtu ambaye nikisoma CV yake ni mtu mzuri sana na makini, ni mmoja kati ya Watanzania wachache ambao walipata nafasi ya kwenda kusomea madawa ya kulevya”.

Pia Mbunge uyo alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kukabidhisha majina yale, anaamini kabisa uchunguzi wa kina utafanyika, kwa watakao kutwa na hatia iliongezea washughulikiwe ili jamii yetu iwe salama.

 

Video: Majaliwa awasha moto Kiteto, amtaka DC, DED kujibu kero za wananchi Jumamosi
Arsene Wenger: Hatopendeza Tukipoteza Tena Dhidi Yao