Katibu Mwenezi wa zamani wa TANU, na Mbunge mstaafu, Faustine Masha amesema ni vigumu katika nchi ambazo zimeruhusu mifumo ya kidemokrasia kufanikisha Mfumo wa  siasa ya Ujamaa na kujitegemea kwa kile alichodai kuwa hakuna uvumilivu wa kisiasa, hayo yaliongelewa jana wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Azimio la Arusha.

Ameeleza ujamaa na kujitegemea ungeweza kufanikiwa iwapo nchi ingeendelea katika mfumo wa chama kimoja, lakini kwa kuruhusu vyama vingi, falsafa hiyo itachukua muda kueleweka.

Masha ametilia mkazo kwa kusema katika nchi ya kidemokrasia jamii inaishi kwa kukosoana hali ambayo haina nafasi katika nchi za kijamaa, viongozi wakikosa uvumilivu wa kupokea kauli za kushutumiwa na kukosolewa ni wazi kuwa hakutakuwa na misingi ya ujamaa.

Amesema Mwalimu Nyerere aliamini katika aujamaa na kujitegemea kwani ndio njia pekee ya kuongeza uzalishaji katika nchi na watu wake si kutegemea watu wa nje.

Kwa upande wa Profesa mstaafu wa chuo Kikuu cha Makerere, Ahmed Mohiddin ameeleza pamoja na changamoto zilizopo nchini bado Tanzania kuna chembechembe ya Azimio la Arusha.

Mwalimu alitamani Afrika iishi katika misingi ya utawala wa Afrika na si kuiga tawala za nje ila hakueleweka hali ambayo inatutafuna hadi sasa,” amesema Profesa Ahmed Mohiddin.

Na mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Abraham Lipumba amesema Azimio la Arusha lilikuwa na misingi ya kusaidia mshikamano wa watu hivyo ni vyema kukawa na mjadala wa pamoja ili kuirejesha nchi katika misingi hiyo.

 

 

 

Video: Mauaji ya watu watatu, Waziri Mwigulu atoa tamko
Afrika Yapendekeza Kuongezewa Timu Kombe la Dunia