Uongozi wa klabu ya Everton umetajaribu kumsajili mshambuliaji na nahodha wa Man Utd Wayne Rooney, mwishoni mwa msimu huu ili kunusuru hali inayomfika ya kushindwa kucheza katika kikosi cha kwanza

Gazeti la Daily Mirror limeripoti kuwa, The Toffees walijaribu mpango huo wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi uliopita, lakini walishindwa kufuatia mkazo uliowekwa na viongozi wa Man Utd wa kutotaka kumuuza Rooney.

Everton wanaamini Rooney bado anaipenda klabu hiyo, ambayo  ilimkuza kabla ya kutimikia Old Trafford mwaka 2004, na hawezi kukataa kurejea Goodison Park.

Meneja wa Everton Ronald Koeman amekiri mbele ya waandishi wa habari kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, na amekua miongoni mwa watu wanaoushinikiza uongozi wa juu kuhakikisha wanatuma ofa mwishoni mwa msimu huu.

“Nafikiri jambo hili linawezekana kwa sababu kila mchezaji anahitaji kucheza katika kikosi cha kwanza, tukifanikiwa kumsajili nina uhakika mambo yatakua mazuri kwa sababu kila mtu anafahamu umuhimu wa Rooney,” Alisema meneja huyo kutoka Uholanzi Dutchman.

“lengo letu ni kumsaidia mchezaji ili aendelee kutimiza ndoto zake za kucheza kwa kujituma na kupata mafanikio, hapa ni nyumbani kwa Rooney, aliondoka akiwa na umri mdogo, na leo akiamua kurudi bado itakiwa faraja kwa mashabiki, kwani atalazimika kumaliza soka lake akiwa hapa.” Aliongeza Koeman

Wema Sepetu aitosa CCM na kujiunga Chadema
Hussein Machozi kurejea na kishindo cha ‘Nipe Sikuachi’ na Man Water