Mama mmoja anayefahamika kwa jina la Neema Mwita, aliyepata mkasa mkubwa na wakusikitisha wa kuunguzwa kwa maji ya moto amepata msaada wa matibabu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na majeraha yanayomtesa.
Neema Mwita alipatwa na mkasa huo wa kuunguzwa kwa maji ya moto na mumewe mwaka 2015 na kupata majeraha makali ambayo licha ya kupata matibabu kutokana na msaada wa wasamalia wema bado hali yake haipo sawa hivyo Rais Magufuli ametoa msaada wa matibabu kwa mama huyo. Rais amesisitiza pia hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya kitendo hicho pamoja na vitendo vingine vya unyanyasaji.
Mama huyo akiongea kwa uchungu mkali na Rais Magufuli kupitia simu ya mkononi amemshukuru sana Rais Magufuli kwa msaada huo. Bofya hapa kutazama maongezi ya Rais Magufuli na Neema, pia simulizi ya mkasa uliompata Neema