Serikali ya China imeitaka Marekani kuimarisha juhudi zake za mahusiano kwa kutatua mgogoro uliopo kati yake na Korea Kaskazini ili kuweza kuendeleza ushirikiano wa kibiashara.

Aidha, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China, Geng Shuang amesema kuwa Washington na Pyongyang zinatakiwa kuchukua majukumu makubwa zaidi katika kutafuta suluhu kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini huku China ikiunga mkono juhudi hizo.

Hatua hiyo ya China imekuja mara baada ya kupiga marufuku uagizaji wa makaa kutoka Korea Kaskazini hatua inayoonyesha kuathiri uchumi unaoyumba yumba wa taifa la Korea Kaskazini.

Hata hivyo rais wa Marekani Donald Trump wiki iliyopita alisema kuwa China inawezakufanya mengi ili kutatua mgogoro huo kama ikitaka.

Askofu Mokiwa alonga, asema mwenye ushahidi ajitokeze
Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za ujuzi