Mshambuliaji Sergio Aguero huenda akaondoka Man City mwishoni mwa msimu huu na kurejea nchini Hispania, kufuatia mipango inayosukwa na viongozi wa Real Madrid.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, Real Madrid wamejipanga kumsajili mshambuliaji huyo kwa ada ya Pauni milioni 60, ambayo inaaminika haiwezi kukataliwa na Man City.

Real Madrid wanaamini endapo watafanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo kutoka nchini Argentina, watakua wametimiza agizo la meneja wao Zinedin Zidane ambaye anataka kuiboresha safu ya ushambuliaji kwa msimu ujao wa.

Aguero, mwenye umri wa miaka 28, alianza kuhusishwa na mpango wa kutaka kuihama Man City tangu alipoanza kupata changamoto za kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola, kufuatia ujio wa mshambiliaji kutoka nchini Brazil, Gabriel Jesus.

Hata hivyo kwa sasa Aguero anapata nafasi ya kucheza, baada ya kuumiwakwa Jesus ambaye huenda akashindwa kurejea uwanjani hadi mwishoni mwa msimu huu.

Gazeti hilo limeongeza, Aguero tayari ameshafanya mazungumzo na Pep Guardiola, kuhusu mustakabali wake klabuni hapo kwa kutaka athibitishiwe kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini hajapatiwa majibu mpaka sasa.

Aguero aliondoka Hispania mwaka 2011 akitokea Altetico Madrid, na kujiunga na Man City kwa ada ya Pauni milioni 38.

Ligi Kuu Ya Tanzania Bara
Ratiba Kamili Ya Mechi Za Ligi Kuu Ya Wanawake Tanzania Bara