Mpango wa kuondoka Etihad Stadium kwa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero huenda ukawa sahihi, kutokana na uongozi wa Man city kushindwa kuzungumza na mchezaji huyo kuhusu mustakabali wake.

Aguero ameviambia vyombo vya habari kuwa, mpaka sasa hakuna dalili zozote za mazungumzo ya mustakabali wake klabuni hapo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amekua katika wakati mgumu wa kutambua mipango yake ya baadae klabuni hapo, anakabiliwa na changamoto ya kucheza katika kikosi cha kwanza, hasa baada ya baada ya kusajiliwa kwa kinda la miaka 19 kutoka nchini Brazil Gabriel Jesus mwezi uliopita.

Jesus ambaye kwa sasa ni majeruhi, anapewa kipaumbele cha kucheza katika kikosi cha kwanza tangu alipowasili na kumuweka benchi Aguero.

Hata hivyo Pep Guardiola amewahi kuwaambia waandishi wa habari kuwa, bado ana mipango mizuri ya Aguero, na asingependa kumuona anaondoka klabuni hapo.

Mkataba wa Aguero unatarajia kufikia kikomo mwaka 2020, na unatoa nafasi ya kusajiliwana klabu yoyote mwishoni mwa msimu huu.

Tayari magwiji wa soka mjini Madrid (Real Madrid) wameshaonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.

Scholarships with March 2015 deadlines
Man Utd Kuamua Hatma Ya Michael Carrick