Mama ongea na mwanao ni kampeni iliyoendeshwa kipindi cha uchahuzi wa rais 2015, ambapo wasanii mbalimbali waliungana kupigania chama cha Mapinduzi CCM, Steven Nyerere akisaidiana na Wema Sepetu wakiwa viongozi wa kampeni hiyo walizungunguka nchi zima kupigania CCM kuendelea kuwa madarakani.
Katika kampeni hiyo kila msanii alihaidiwa kulipwa laki tano mara baada ya kumaliza kuzunguka kila mkoa mmoja, lakini kwa baadhi ya maelezo ya wasanii mara tu baada ya kumaliza mkoa mmoja hawakuweza kukabidhiwa fedha zao walizoahidiwa kabla ya kampeni.
Utata umezuka katika wasanii walioshiriki kampeni ya mama ongea na mwanao kwani wasanii hao wametengeneza tabaka wapo wanaodai kulipwa fedha zao pia wapo wanaodai kutolipwa fedha zao.
Hivyo baadhi ya wasanii wameungana na kumtaka mchekeshaji Steve Nyerere kuonesha mkataba wa malipo ambao ulitolewa na CCM lengo kubwa ni kukata mzizi wa fitina baina ya wasanii, wananchi na uongozi mzima wa CCM.
Pia wameomba Viongozi wa CCM kumbana Steve Nyerere, aeleze ni wapi fedha za wasanii hao alikozipeleka kwa sababu kitendo cha kudhulumu fedha hizo baadhi ya wananchi wanafikiri kimefanywa na chama cha mapinduzi CCM wakati mzigo wote ulikabidhiwa kwa Steve Nyerere.
Steve alikua na la kujibu kuhusiana na tuhuma hizo na kudai kuwa wote ambao hawakulipwa fedha taslimu ni wale ambao walikuwa hawana mkataba ni wabeba mizigo .
‘’Alikwambia ana mkataba, huyo alikuwa hakuajiriwa na alikuwa mbeba mizigo na wabeba mizigo wote wameshalipwa hakuna anayedai ‘’.
Hivyo Nyerere aliwaomba wananchi kupuuzia tuhuma hizo kwani hazina ukweli ndani yake.