Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini, Zitto Kabwe ametoa maoni yake kuhusu uteuzi wa mke wa rais mstaafu, Salma Kikwete na kusema jibu ambalo anaweza kuweka wazi kwa umma ni kwamba Salma Kikwete ana haki zote kama Mtanzania mwengine yeyote kuteuliwa ama kuchaguliwa kwa mujibu wa Katiba yetu. Hivyo amesema kuwa uteuzi wake ni kama teuzi nyengine.
”Kuolewa kwake na aliyekuwa Rais, hakumwondolei yeye haki zake za kikatiba. Kama mwenyewe ataridhia ninamtakia kila la kheri katika kazi yake mpya”. Amesema Zitto Kabwe
Japokuwa wapo viongozi ambao bado hawajakubaliana na uteuzi huo na kuhoji maswali mengi juu ya uteuzi wa Salma Kikwete.
Mmoja wa wanasisa na Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation Khamis Mgeja kwa upande wake alimtaka mama Salma Kikwete kuiga mfano wa Regina Lowassa ambaye alikataa nafasi ya Ubunge Viti Maalamu katika chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Na baadhi ya wananchi walihojiwa kuhusu uteuzi huo na kutoa hoja zao, Naye Mauld Omary, amesema ”Bunge hili linakwenda kuwa la kindugu sipati picha pale mtoto wake Ridhiwani Kikwete akisimama kuchangia hoja na mama yake anasimama kuchangia, akizomewa au kutolewa maneno machafu itakuwa aibu kubwa kwa mke wa rais mstaafu,”.