Sakata la tokomeza Pombe aina ya viroba lilioanzishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, limeshika nafasi kubwa nchini baada ya wazalishaji wa kilevi hicho kuomba kuongezewa muda wa kusambaza Pombe aina hiyo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kiwanda cha Truebelly Industry, Godwini Mungure alipokutwa katika ziara kushtiukiza inayofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Aidha, Mungure ameiomba Serikali iongeze muda ili waweze kupata nafasi ya kuweza kusambaza bidhaa zao ambazo tayari walisha ripia kodi ya kufanya biashara katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Tunaiomba Serikali itufikirie angalau tumalize bidhaa hii, turudishe tu mtaji wetu kwa sababu imekuwa ni ghafla sana hatujapata faida yeyote,”amesema Mungure.
Hata hivyo, Serikali inaaendelea na zoezi la kutokomeza pombe aina ya viroba ambayo imekuwa ikitumiwa na nguvu kazi kubwa ya vijana .