Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem amezindua mradi wa visima vya maji kwajili ya kusaidia wanafunzi 5600 wa shule tatu za msingi Yombo jijini Dar es salaam.
Akiongea na wanafunzi hao pamoja na wadau waliojitokeza katika uzinduzi huo, Balozi alisema wameamua kusaidia shule hizo ili kujenga mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu.
“Tunashukuru sana kuwa hapa, ni furaha yetu mradi wetu umekamilika, tunaimani utasaidia wanafunzi wengi pamoja na kujenga mazingira mazuri kwajili ya kujisomea. Kwahiyo kama ubalozi tumedhamiria kusaidia shule mbalimbali kama tulivyofanya hapa ili kuboresha elimu,” alisema balozi huyo.
Kwa upande wa Mrisho Mpoto ambaye alizungumza kuhusu udinduzi huyo, aliwataka wanafunzi kuyatumia vizuri mazingira hayo kwa manufaa wao.
“Kila mwanafunzi hapa ana ndoto yake, mimi ningependa muyatumie vizuri haya mazingira, kwa sababu kuna wanafunzi wanataka haya mazingira halafu wanakosa, kwahiyo ni vyema mkajua hapa kimewaleta nini,” alisema Mpoto.