Akiendelea na ziara yake Mkoani Lindi, Rais Dkt Magufuli  amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo na kutoa maagizo ili kuhakikisha wananchi wananufaika na jitihada za Serikali za kuboresha maisha yao.
Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Godfrey Zambi kumnyang’anya pasipoti ya kusafiria Mkandarasi anayeshughulikia Mradi wa Maji wa Ngapa hadi hapo atakapokamilisha mradi huo.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokwenda kukagua mradi huo wa maji ambao hadi sasa umetumia miaka 6 kujengwa lakini bado haijakamilika. Pamoja na kuagiza pasipoti ya mkandarasi ichukuliwe, Rais Magufuli amempa miezi miwili mkandarasi huyo kuhakikisha mradi unakamili huku RC Zambi akiwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mkandarasi hatoki eneo hilo la mradi.
Aidha, mradi huo unaotarajiwa kumaliza tatizo la maji mkoani Lindi umegharimu sh. bilioni 29 ambapo hadi sasa mkandarasi amelipwa bilioni 21.
Hata hivyo, Rais Magufuli anatarajiwa kukamilisha ziara yake mkoani Lindi ambapo ataanza safari ya kwenda mkoani Mtwara atakapofanya ziara yake Jumamosi na Jumapili. Katika kuhitimisha ziara yake ya siku nne katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, Rais Magufuli na anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

Wema Sepetu amuahidi ‘jambo’ Lema baada ya kutoka gerezani
Video: Godbless Lema aitikisa Arusha, JPM azuia pasipoti za wakandarasi