Wataalamu wa kusoma ishara na matamshi wamepingana na baadhi ya wadau wa soka duniani ambao walitafsri tofauti ushangiliaji wa mshambuliaji, Lionel Messi wakati wa mchezio wa ligi ya nchini Hispania dhidi ya Celta Vigo.

Messi alionyensha ishara wa kupiga simu baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo huo, ambao ulimalizika kwa FC Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao matano kwa sifuri.

Ilidaiwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania alionyesha kitendo cha kupiga simu alipokua akishangilia, kwa lengo la kuwatumia ujumbe viongozi wa FC Barcelona kuhusu mazungumzo ya mkataba wake mpya.

Majibu ya wataalamu yameonyesha kuwa, Messi hakua na maana mbaya kwa viongozi wake, na baadae alipoulizwa alikiri kufanya kitendo hicho kwa ajili ya binamu yake Augustin, ambaye alikua akimsaka kwa njia ya simu kwa siku nzima ya jumamosi bila mafanikio.

Mshambuliaji huyo amesema alifanya hivyo kwa kuamini Augustin alikua akifuatilia mchezo dhidi ya Celta Vigo na alimfikishia ujumbe kwa kumuambia kwa vitendo kwa nini alikua hapokei simu yake kutwa nzima.

Messi bado hajakubali kusaini mkataba mpya, kwa kushinikiza athibitishiwe baadhi ya mambo na uongozi wa klabu hiyo, hususan suala la mrithi wa meneja wa sasa Luis Enrique ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Endapo ataendelea na msimamo wake wa kutosaini mkataba mpya Messi atakua huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote kuanzia mwezi Januari mwaka 2018.

Azam Sports Federation Cup, Zamu Ya Yanga Vs Kiluvya Utd
Antonio Conte Awapa Somo The Blues