Timu ya Simba SC itamenyana na Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Machi 18, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, mabingwa watetezi, Yanga SC iwapo watafanikiwa kuitoa Kiluvya United ya Pwani kesho watamenyana na Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 18.

Na kama Kiluvya United wataitoa Yanga kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam basi wao ndiyo wataialika Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani Machi 18.

Washindi wa pili wa mwaka jana, Azam FC watamenyana na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Machi 18, wakati Kagera Sugar watamenyana na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba, Bukoba siku hiyo.

Wakati huo huo: Simba SC itamenyana na Polisi Dodoma Jumamosi katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Jamhuri mjini huo.

Mchezo huo umeandaliwa na Chama cha Soka Dodoma (DOREFA) na Simba itautukia kama sehemu ya maandalizi kabla ya kumenyana na Madini FC.

Tony Bellew Afikiria Kustaafu Ndondi
Trump aendelea na msimamo wake kuhusu wahamiaji