Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Australia Ange Postecoglou ametangaza kikosi cha wachezaji 30, ambacho kitaingia kambini, kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya Iraq na United Arab Emirates (UAE).

Katika kikosi hicho, kocha huyo amemuita mkongwe Tim Cahill na Tomi Juric.

Wawili hao walikosa mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Thailand mwezi Novemba mwaka jana, hatua ambayo iliibua lawama kwa mashabiki wa soka la Australia kwa kuhisi endapo wangekuwepo matokeo yangekua mazuri kwao.

Australia watacheza mchezo dhidi ya Iraq Machi 23 kabla ya kukutana na UAE mjini Sydney Machi 28.

Vibaraka Wa Perez Watafuta Nyumba Ya Eden Hazard
Arsene Wenger: Klabu Ipo Katika Muhimili Mzuri