Mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, wamedhamniria kumsajili kiungo mshambuliaji wa vinara wa ligi ya England (Chelsea) Eden Hazard mwiashoni mwa msimu huu.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameshakubali kulifanyia kazi ombi la meneja Zinedine Zidane la kutaka ahakikishe Hazard anakuwa sehemu ya kikosi chake msimu ujao.
Mwandishi wa habari wa Hispania Don Balon amesema Real Madrid wamejipanga kukamilisha usajili wa mchezaji huyo kwa kutumia nafasi ya kuwaweka sokoni James Rodriguez ama Isco ili kupata fedha zitakazowezesha usajili wa Hazard.
Mwandishi huyo amesema thamani ya Hazard huenda ikafikia Euro milioni 70, na kuna uhakika wa mauzo ya washambuliaji hao yakasaidia kupatikana kwa kiasi hicho cha pesa, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.
Don Balon pia amefichua siri nyingine inayohusu mpango wa usajili wa Hazard, kwa kusema tayari vibaraka wa Perez wameanza kutafuta nyumba kwa ajili ya makazi ya mchezaji huyo wa Chelsea.
Balon amesema nyumba inayotafutwa kwa ajili ya Hazard ina thamani ya Euro milioni 6, na ipo karibu na makazi ya wachezaji wengine wa Real Madrid Gareth Bale, Karim Benzema, James Rodriguez, Tony Kroos na Sergio Ramos.